Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Kupitia Email kwa Kiswahili
Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe) Maombi ya kazi kupitia email husaidia yafuatayo: kuokoa gharama kama za uchapaji na usafirishaji kuokoa muda wa barua kutoka kwa muombaji mpaka imfikie mwajiri Kuharakisha pia mawasiliano baada ya maombi kutumwa Kama utaomba kazi kupitia email zingatia yafuatayo: Tumia email yenye majina yako rasmi. Mfano kama wewe ni Daudi Joseph Masanja, email iwe hivi. hefsibageoege@gmail.com, NK. Angalau majina yako mawili yatokee kwenye email ID. Unaweza hata kuongeza namba kama majina yako mawili hayapatikani. Kumbuka hii itaongeza kuaminiwa na mwajiriwa mtarajiwa kuliko kutumia email kama pacomezozoa@gmail.com au djmbuzi@gmail.com mpambanaji@gmail.com NK Tumia pia email zenye kufuata weledi wa kimataifa. Mfano siwashauri watu kutumia email za microsoft, yahoo au zinginezo ambazo zinatumia very offensive security blocking policy. Mfano halisi ni huu email za Microsoft zinaongoza kwa kublock makundi mengi ya email duniani. Kwa hiyo ikitokea ...